Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 161

An-Nisaa 4:161

النساء

وَأَخْذِهِمُ ٱلرِّبَوٰا۟ وَقَدْ نُهُوا۟ عَنْهُ وَأَكْلِهِمْ أَمْوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلْبَـٰطِلِ ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا

Maana

Na kuchukua kwao riba, na ilhali walikwishakatazwa hilo, na kula kwao mali ya watu kwa batili. Basi tumewaandalia makafiri katika wao adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kuchukua kwao riba, nao wamekatazwa, na kula kwao mali ya watu kwa dhulma. Basi tumewaandalia makafiri katika wao adhabu yenye uchungu. [161]

[161] Na kwa sababu ya kupenda kula riba - na Mwenyezi Mungu alikwisha wakataza hayo - na kuchukua mali ya watu kwa njia isiyo ya haki, ndio ikawa adabu ya dini ni kuwazuilia na kula vyakula vilivyo vizuri. Na Mwenyezi Mungu amewawekea hao walio kufuru adhabu yenye kutia machungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa sababu ya kutumia kwao riba ambayo walikatazwa wasitumie na kujihalalishia kwao mali za watu pasi na haki. Na tumewatayarishia waliomkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake adhabu iumizayo huko Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net