Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 160

An-Nisaa 4:160

النساء

فَبِظُلْمٍ مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَـٰتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ كَثِيرًا

Maana

Basi kwa sababu ya dhuluma ya Mayahudi, tuliwaharamishia vitu vizuri walivyohalalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kwa dhulma yao Mayahudi tuliwaharimishia vitu vizuri walivyo halalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu. [160]

[160] Kwa sababu ya udhalimu wao Mayahudi Mwenyezi Mungu amewapa adabu - amewakataza vyakula mbali mbali vilivyo vizuri, vimekuwa kwao ni haramu, na ilhali kwanza vilikuwa halali kwao. Na kwa udhalimu wao wamewazuia watu wengi wasiingie katika Dini ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa sababu ya dhuluma ya Mayahudi kwa madhambi makubwa waliyoyafanya, Allah Mtukufu Aliwaharamishia vyakula vizuri vilivyokuwa halali kwao, na pia kwa sababu ya kuzizuia nafsi zao na kuwazuia wengine wao wasiifuate dini ya Allah Mtukufu iliyo ya sawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net