Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 159

An-Nisaa 4:159

النساء

وَإِن مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِۦ قَبْلَ مَوْتِهِۦ ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا

Maana

Na hawi katika Watu wa Kitabu isipokuwa hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao.[1]

[1] Hakuna hata mmoja katika Watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo) ambaye hatamwamini Isa, amani iwe juu yake, baada ya kuteremka kwake katika mwisho wa zama na kabla ya kufa kwake Isa katika zama hizo. Na Siku ya Kiyama, Isa, amani iwe juu yake, atakuwa shahidi juu ya matendo yao. Yale yanayokubaliana na sheria na yale yanayopingana nayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao. [159]

[159] Na hapana mmojapo katika Watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo) ila atakuja tambua uhakika wa Isa (kuwa ni Nabii wa kweli wa Mwenyezi Mungu, si mwana haramu, wala si mwana wa Mungu) kabla ya kufa kwake, na kuwa yeye Isa ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na atakuja amini imani ambayo haitomfaa kitu, kwa kuwa wakati wake umekwisha pita. Na Siku ya Kiyama Isa atatoa ushahidi juu yao kuwa yeye alifikisha ujumbe, na kuwa yeye ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika hatasalia yoyote, kati ya wale waliopewa Kitabu, baada ya kuteremka ‘Ǐsâ zama za mwisho, isipokuwa atamuamini Nabii ‘Ǐsâ kabla ya kufa kwake, amani imshukie, na siku ya Kiyama Nabii ‘Ǐsâ atakuwa ni shahidi kwamba waliomkanusha walikuwa warongo na waliomuamini walikuwa wakweli.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net