Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 158

An-Nisaa 4:158

النساء

بَل رَّفَعَهُ ٱللَّهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

Maana

Bali Mwenyezi Mungu alimwinua kwenda kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [158]

[158] Bali Mwenyezi Mungu alimtukuza kwake, akamwokoa na maadui zake, wasimsalibu na wasimuuwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda, hashindiki, ni Mwenye hikima katika vitendo vyake. (Taaurati inayo kubaliwa na Mayahudi na Wakristo imesema kuwa anaye kufa kwa kutundikwa msalabani amelaaniwa. Ndio maana Mayahudi wakawa na hamu wamtundike Nabii Isa ili wathibitishe kuwa huyo si chochote ila ni mlaanifu. Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu vipi aachilie jambo hilo liwe kwa Mtume wake?)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Bali Allah Mtukufu Alimpaisha ‘Ǐsâ kwa mwili wake na roho yake akiwa hai na Alimuokoa dhidi ya wale waliokufuru. Na Allah Mtukufu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na mapitisho Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net