An-Nisaa 4:157
النساءوَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا ٱلْمَسِيحَ عِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ ٱللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا ٱتِّبَاعَ ٱلظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًۢا
Na kusema kwao: 'Hakika, sisi tulimuua Masihi Isa, mwana wa Maryam, Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Nao hawakumuua wala hawakumsulubisha, bali walifananishiwa tu. Na hakika wale waliohitilafiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana elimu yoyote nayo isipokuwa ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuua kwa yakini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. [157]
[157] Na Mwenyezi Mungu pia amewaghadhibikia kwa kusema kwao uwongo: Hakika sisi tumemuuwa Masihi Isa bin Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na kweli ya yakini ni kuwa hawakumuuwa kama wanavyo zua. Wala hawakumsulubu kama wanavyo dai. Lakini walifananishiwa, nao wakadhani kuwa wamemuuwa na wamemsalibu. Na hakika walimuuwa na kumsalibu aliye shabihiana naye. Nao wakaja kukhitalifiana baada ya hayo, kuwa aliyeuwawa ni Isa au mtu mwengine? Na wote hao, kwa hakika, wamo katika shaka tu juu ya jambo hilo. Kweli iliyopo ni kuwa hawana ujuzi nayo mambo haya, ila ni dhana tu. Kabisa hawakumuuwa Isa. (Wataalamu wa Biblia mpaka hii leo wamo kuzozana katika jambo hili. Mwenye kuzichungua Injili zinazo kubaliwa na Wakristo ataona kuwa hazina uthibitisho kuwa aliye salibiwa ndiye Yesu, au hata huyo naye alikufa msalabani au la.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na- pia tuliwalaani- kwa sababu ya neno lao, kwa njia ya kukejeli na shere, «Sisi tumemuua Al- Masîh,, ‘Ǐsâ mwana wa Maryam, mjumbe wa Allah Mtukufu.» Na wala wao hawakumuua ‘Ǐsâ wala hawakumsulubu, bali walimsulubu mwanamume aliyefanana naye kwa kudhani kwao kuwa yeye ndiye ‘Ǐsâ. Na yoyote aliyedai kwamba walimuua, miongoni mwa Mayahudi na pia wale waliomsalimisha kwao, miongoni mwaWanaswara, wote hao wako kwenye shaka na kuchanganyikiwa; hawana ujuzi wowote isipokua ni kufuata dhana tu, na wala hawana yakini ya kuwa walimuua, bali wana shaka nalo hilo na wanalidhania tu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net