Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 156

An-Nisaa 4:156

النساء

وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَـٰنًا عَظِيمًا

Maana

Na kwa kufuru zao na kusema kwao juu ya Maryam uongo mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa. [156]

[156] Na Mwenyezi Mungu amewaghadhibikia Mayahudi kwa sababu ya kufru yao na kumzulia Maryam uzushi mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na vile vile tuliwalaani kwa sababu ya ukafiri wao na kumzulia kwao Maryam urongo kwa yale waliyomsingizia nayo ya uzinifu na hali yeye yupo mbali na hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net