Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 155

An-Nisaa 4:155

النساء

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَـٰقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَقَتْلِهِمُ ٱلْأَنۢبِيَآءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌۢ ۚ بَلْ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا

Maana

Basi kwa sababu ya kuvunja kwao maagano yao, na kuzikufuru kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: 'Nyoyo zetu zimefumbwa'; bali Mwenyezi Mungu ameziziba kwa kufuru zao, basi hawaamini isipokuwa kidogo tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi zao, na kuzikataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri kwa kufuru zao, basi hawaamini ila kidogo tu. [155]

[155] Mwenyezi Mungu akawakasirikia kwa sababu ya kuvunja agano hili, na kuzikataa ishara za Mwenyezi Mungu, na kwa kuwauwa Manabii kwa dhulma, na kuendelea katika upotovu wao kwa kusema: Nyoyo zetu zimefungwa hazikubali hayo unayo tuitia! Nao hawasemi kweli katika kauli yao hiyo, bali Mwenyezi Mungu amezifuta nyoyo zao kwa ukafiri wao, basi ni wachache tu kati yao wanao amini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tukawalaani kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi, kukanusha kwao aya za Allah Mtukufu zinazojulisha ukweli wa Mitume Wake, kuua kwao Manabii wa Allah Mtukufu kwa maonevu na uadui na kwa kusema kwao, «Nyoyo zetu zimezibwa kwa vifiniko, hatuyafahamu uyasemayo.» Bali Allah Mtukufu ameziziba kwa sababu ya ukafiri wao. Kwa hivyo, hawataamini isipokuwa Imani isiyowafaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net