An-Nisaa 4:154
النساءوَرَفَعْنَا فَوْقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَـٰقِهِمْ وَقُلْنَا لَهُمُ ٱدْخُلُوا۟ ٱلْبَابَ سُجَّدًا وَقُلْنَا لَهُمْ لَا تَعْدُوا۟ فِى ٱلسَّبْتِ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَـٰقًا غَلِيظًا
Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingieni mlangoni kwa kusujudu. Na tukawaambia: Msikiuke mipaka kuhusiana na Siku ya Sabato (Jumamosi). Na tukachukua kwao agano lililo madhubuti.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingilieni mlangoni kwa unyenyekevu. Na tukawaambia: Msiivunje Siku ya Sabato (Jumaa mosi). Na tukachukua kwao ahadi iliyo madhubuti. [154]
[154] Mwenyezi Mungu akaunyanyua mlima juu ya Wana wa Israili ili kuwatisha kwa kule kuikataa kwao sharia ya Taurati, mpaka wakaikubali. Akachukua kwao agano, na akawaamrisha waingie mjini hali wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Wala wasiyakiuke aliyo waamrisha kushika ibada katika siku ya Sabato, yaani Jumaamosi.(Imeitwa "Sabt" Kiarabu, "Shabbath" Kiyahudi, "Sabbath" Kiingereza, na "Sabato" Kiswahili, maana yake "Mapumziko" kwa kuwa ni siku ya mapumziko kwa Mayahudi.) Na Mwenyezi Mungu alichukua kwao ahadi ya nguvu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukaliinua juu ya vichwa vyao jabali la Tûr walipokataa kujilazimisha na ahadi iliyotiliwa mkazo waliyoitoa ya kuwa watazitumia hukumu za Taurati. Na tukawaamrisha waingie lango la Bait al-Maqdis hali ya kusujudu, nao wakaingia wakijikokota kwa matako yao. Na tukawaamrisha wasifanye uadui kwa kuvua siku ya Jumamosi, wakafanya uadui hivyo hivyo na wakavua. Na tukachukua kutoka kwao ahadi ya mkazo, pia waliivunja hivyo hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net