Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 153

An-Nisaa 4:153

النساء

يَسْـَٔلُكَ أَهْلُ ٱلْكِتَـٰبِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَـٰبًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا۟ مُوسَىٰٓ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوٓا۟ أَرِنَا ٱللَّهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ ٱتَّخَذُوا۟ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَءَاتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَـٰنًا مُّبِينًا

Maana

Watu wa Kitabu wanakuuliza uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika, walikwishamuuliza Musa makubwa zaidi ya hayo. Walisema: 'Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi.' Kwa hivyo, radi ikawapiga kwa dhuluma yao hiyo. Kisha wakamchukua ndama kumwabudu, baada ya kwishawajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa hoja zilizo dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri. [153]

[153] Ewe Mtume! Watu wa Kitabu, yaani Mayahudi wapendao kuudhi, wanakutaka ulete dalili ya ukweli wa unabii wako. Uwaletee kitabu makhsusi kiwateremkie kutoka mbinguni kithibitishe ukweli wa utume wako, na kiwatake wakuamini na kukut'ii! Ukiyaona makuu hayo wayatakayo, wewe usifanye haraka. Kwani wenzao walio tangulia walifanya kero vile vile, wakamtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walimwambia: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu tumwone kwa macho. Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa lile kero lao na dhulma yao kwa kuwapiga radi iliyo wateketeza!! Kisha watajie hawa watu kosa kubwa zaidi na ovu zaidi, nalo ni pale walipo mfanya ndama kuwa ni Mungu wao, wakamwacha Mwenyezi Mungu aliye waumba. Haya baada ya kwisha ona dalili zote alizo zionyesha Musa kwa Firauni na kaumu yake!! Kisha juu ya hayo Mwenyezi Mungu akawakunjulia usamehevu wake kwao, na Mwenyezi Mungu akampa nguvu Musa kwa hoja zilio wazi, na neno madhubuti.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanakutaka Mayahudi, ewe Mtume, uwaonyeshe miujiza mfano wa miujiza ya Mûsã iwe ni ushahidi kwako kuwa ni mkweli, nao ni uwateremshie kurasa zitokazo kwa Allah Mtukufu hali ya kuwa zimeandikwa, kama vile Mûsã alivyoleta mbao kutoka kwa Allah Mtukufu. Usione ajabu, ewe Mtume, kwani wakale wao walimtaka Mûsã, amani imshukie, awaletee makubwa zaidi. Walimtaka Awaonyeshe Allah Mtukufu waziwazi, hapo wakateremshiwa moto uliowaua kwa sababu ya kuzidhulumu nafsi zao walipolitaka jambo ambalo si haki yao. Na baada ya Allah Mtukufu kuwahuisha, baada ya kufa kwao, na wakaishuhudia miujiza iliyo waziwazi, kutoka kwa Mtume Mûsã, inayopinga katakata ushirikina, waliabudu kigombe badala ya Allah Mtukufu. Kisha tuliwasamehe kosa lao la kuabudu ndama kwa sababu ya kutubia kwao na tukampa Mûsã hoja kubwa zilizotilia nguvu ukweli wa utume wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net