An-Nisaa 4:152
النساءوَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَلَمْ يُفَرِّقُوا۟ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُو۟لَـٰٓئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Na wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala hawakumfarikisha yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu. [152]
[152] Na ama wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala hawakumkanusha hata mmoja wapo kati yao, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atawalipa malipo makubwa kwa ajili ya Imani yao iliyo kamilika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira kwa wenye kutubu, na ni Mwenye kuwarehemu waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale walioukubali upweke wa Allah Mtukufu na wakautambua unabii wa wajumbe Wake wote na wasimbague yoyote kati yao na wakaifuata kivitendo sheria ya Allah Mtukufu, hao Atawapa malipo yao na thawabu zao kwa kumuamini kwao Yeye na Mitume Wake. Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net