An-Nisaa 4:15
النساءوَٱلَّـٰتِى يَأْتِينَ ٱلْفَـٰحِشَةَ مِن نِّسَآئِكُمْ فَٱسْتَشْهِدُوا۟ عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا۟ فَأَمْسِكُوهُنَّ فِى ٱلْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّىٰهُنَّ ٱلْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ ٱللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلًا
Na wale ambao wanafanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, washuhudisheni watu wanne katika nyinyi. Watakaposhuhudia, basi wazuieni majumbani mpaka wafishwe na mauti au Mwenyezi Mungu awafanyie njia nyengine.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambao wanafanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, washuhudizieni watu wane katika nyinyi. Watakapo shuhudia, basi wazuieni majumbani mpaka wafishwe na mauti au Mwenyezi Mungu awatolee njia nyengine. [15]
[15] Na wale wanawake wanao zini wakishuhudiwa na mashahidi wanaume wane walio waadilifu, basi wazuieni wasitoke nyumbani kwa ajili ya kuwalinda na kuzuia usiendelee ufisadi na shari mpaka wafe, au Mwenyezi Mungu awafungulie njia ya maisha yaliyo sawa kwa kuolewa na kutubu. (Wafasiri wengine wanasema hukumu hii ni kwa wanawake wanao fanya mambo machafu wenyewe kwa wenyewe, sio ya zina baina ya mwanamke na mwanamume. Kwa kuhifadhi heshima ya wanawake inalazimu wapatikane mashahidi wane, badala ya wawili, walio ona kitendo khasa, sio kuwatuhumu watu kwa jambo ovu kama hilo bila ya mashahidi wane walio shuhudia kwa macho yao.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wanaozini katika wanawake wenu, washuhudisheni kwao, enyi viongozi na makadhi, wanaume wanne waadilifu miongoni mwa Waislamu, Na iwapo watatoa ushahidi juu yao kwa hilo, wazuieni, wanawake hao, majumbani mpaka yamalizike maisha yao kwa kufa au Allah Mtukufu awape njia ya kuwaokoa na hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net