Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 14

An-Nisaa 4:14

النساء

وَمَن يَعْصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُۥ يُدْخِلْهُ نَارًا خَـٰلِدًا فِيهَا وَلَهُۥ عَذَابٌ مُّهِينٌ

Maana

Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, naye ana adhabu ya kudhalilisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha. [14]

[14] Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akaikiuka mipaka aliyo iweka Mwenyezi Mungu, na huku akihalalisha kukiuka huko basi mtu huyo atalipwa Moto, na humo atakaa milele, akiadhibiwa mwili wake juu ya kuadhibiwa roho yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kumuasi Allah Mtukufu na Mtume Wake, kwa kuzikanusha hukumu za Allah Mtukufu na kuzikiuka Sheria Zake kwa waja Wake, kwa kuzibadilisha au kuacha kuzitumia, huyo Atamuingiza Motoni, adumu humo; na atapata adhabu ya kumfanya mnyonge.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net