Az-Zumar 39:68
الزمروَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ إِلَّا مَن شَآءَ ٱللَّهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ
Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipokuwa aliyemtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara nyingine. Hapo watainuka wawe wanangojea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea. [68]
[68] Na litapulizwa barugumu kwa yakini, na watakufa walioko mbinguni na katika ardhi ila anaye mtaka Mwenyezi Mungu kumuakhirisha mpaka wakati mwengine. Kisha litapulizwa mara nyengine, na hapo wote watainuka kutoka makaburini mwao, wakingojea watafanywa nini? Hilo barugumu (S'ur) kilugha, ni tarumbeta, mbiu, siwa, parapanda. Barugumu inalo tusimulia Qur'ani ni katika mambo ya ulimwengu usio onekana, hatujui lilivyo na hakika yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kutapulizwa kwenye baragumu na hapo atakufa kila aliye kwenye mbingu na ardhi, isipokuwa anayemtaka Allah Mtukufu asife. Kisha Malaika Atapuliza mara ya pili kwenye baragumu akitangaza kufufuliwa viumbe wapate kuhesabiwa mbele ya Mola wao, na wakitahamaki wao wamesimama kutoka makaburini mwao wanangojea yale Atakayowafanyia Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net