Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 67

Az-Zumar 39:67

الزمر

وَمَا قَدَرُوا۟ ٱللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِۦ وَٱلْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُۥ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَٱلسَّمَـٰوَٰتُ مَطْوِيَّـٰتٌۢ بِيَمِينِهِۦ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Maana

Na wala hawakumheshimu Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kuheshimiwa. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kiume. Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Subhanahu wa Taa'la Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayo mshirikisha nayo. [67]

[67] Washirikina hawakumtukuza Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki utukufu wake, wala hawakumjua kama anavyo stahiki kujuulikana, kwa kuwa wamemshirikisha pamoja naye wenginewe, na wakamtaka Mtume naye aingie katika ushirikina, na hali ardhi yote ni milki yake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa, kama zinavyo kunjwa nguo, katika mkono wake wa kulia. Mwenyezi Mungu ametakasika na kila upungufu, na ametukuka vikubwa mno na vyote hivyo wanavyo mshirikisha naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa washirikina hawakumuadhimisha Allah Mtukufu vile Anavyostahiki kuadhimishwa, kwa kuwa wamemuabudu asiyekuwa Yeye pamoja na Yeye miongoni mwa wale wasionufaisha wala kudhuru, wakamfanya muumbwa, pamoja na uelemevu wake, kuwa ni sawa na Muumba Mtukufu, Ambaye kotokana na uwezo Wake mkubwa ni kwamba ardhi yote itakuwa iko mkononi Mwake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa kwa mkono Wake wa kulia. Ametakasika Allah Mtukufu na kile wanachomshirikisha nacho hao washirikina. Katika aya hii pana dalili ya kuthibitisha kushika kwa mkono, mkono wa kulia na kukunja kwa Allah Mtukufu kama vile inavyolingana na haiba Yake na utukufu Wake bila kueleza namna gani wala kufananisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net