Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 69

Az-Zumar 39:69

الزمر

وَأَشْرَقَتِ ٱلْأَرْضُ بِنُورِ رَبِّهَا وَوُضِعَ ٱلْكِتَـٰبُ وَجِا۟ىٓءَ بِٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَقُضِىَ بَيْنَهُم بِٱلْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Maana

Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. [69]

[69] Na ardhi itang'ara siku hiyo kwa nuru ya Muumba wake na Mmiliki wake. Na kitatayarishwa Kitabu kilicho sajiliwa ndani yake vitendo vyao, na watahudhurishwa Manabii na mashahidi wapate kuwashuhudia viumbe vyote, na wapambanuliwe baina ya viumbe kwa uadilifu, na wala hawatadhulumiwa kwa kupunguziwa thawabu wala kuzidishiwa adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ardhi itatoa mwangaza Siku ya Kiyama, atakapojitokeza Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, ili kutoa hukumu, na hapo Malaika wautandaze ukurasa wa kila mtu, na Mitume waletwe na mashahidi wa kila ummah, ili Allah Mtukufu Awaulize manabii kuhusu ufikishaji ujumbe kwa ummah wao na majibu waliopata kutoka kwao. Kadhalika waje ummah wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu rehema na amani zimshukie, ili kuutolea ushahidi ufikishaji wa Mitume waliotangulia kwa ummah zao iwapo watakataa kuwa walifikishiwa. Na hapo ushahidi uthibiti juu ya ummah zote, na Allah Mtukufu Atoe hukumu baina ya waja kwa uadilifu uliotimia. Na wao hawatadhulumiwa kitu chochote kwa kupunguziwa thawabu au kwa kuongezewa mateso.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net