Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 60

Az-Zumar 39:60

الزمر

وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ تَرَى ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ ۚ أَلَيْسَ فِى جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ

Maana

Na Siku ya Kiyama utawaona waliomsingizia uongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je, si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Siku ya Kiyama utawaona walio msingizia uwongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je! Si katika Jahannamu makaazi ya wanao takabari? [60]

[60] Na Siku ya Kiyama utawaona walio mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, wakamkhusisha yasiyo kuwa yake, nyuso zao zimesawjika kwa huzuni na majonzi. Hakika Jahannamu ndio makaazi ya wenye kiburi wakaikataa Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Siku ya Kiyama utawaona hao wakanushaji, waliomsifu Mola wao kwa sifa zisizolingana na Yeye na wakamnasibisha Yeye na mshirika na mwana, nyuso zao zimekuwa nyeusi. Si ndani ya Jahanamu kuna mashukio na makao kwa aliyemfanyia Allah Mtukufu kiburi akakataa kumpwekesha na kumtii? Ndio.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net