Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 59

Az-Zumar 39:59

الزمر

بَلَىٰ قَدْ جَآءَتْكَ ءَايَـٰتِى فَكَذَّبْتَ بِهَا وَٱسْتَكْبَرْتَ وَكُنتَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Wapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri! [59]

[59] Utayapata wapi, ewe mwenye majuto! Mafunzo yangu yalikujia katika ndimi za Mitume, nawe ukayakanusha, na ukajiona bora, ukakataa kuyafuata, na ukawa katika dunia yako miongoni mwa wenye kushikilia ukafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Maneno siyo kama unavyosema, Kwa hakika aya zangu zilizo wazi zenye kuitolea ushahidi haki zilikujia ukazikanusha, ukazifanyia kiburi usizikubali na usizifuate na ukawa ni miongoni mwa wenye kumkanusha Allah Mtukufu na Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net