Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 58

Az-Zumar 39:58

الزمر

أَوْ تَقُولَ حِينَ تَرَى ٱلْعَذَابَ لَوْ أَنَّ لِى كَرَّةً فَأَكُونَ مِنَ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Au ikasema inapoona adhabu: Lau kuwa ningelipata fursa nyingine, ningelikuwa miongoni mwa wafanya mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au ikasema inapo ona adhabu: Lau kuwa ningeli pata fursa nyengine, ningeli kuwa miongoni mwa wafanya mema. [58]

[58] Au iseme nafsi ile yenye dhambi itapo ona adhabu: Laiti ningeli rejeshwa duniani, nikawa katika wanao tengeneza imani yao na vitendo vyao!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au ikasema, itakapoiona adhabu ya Allah Mtukufu imeizunguka Siku ya Kiyama, ‘Natamani nipatiwe nafasi ya kurudi kwenye maisha ya kilimwengu nikawa huko ni miongoni mwa wenye kufanya wema kwa kumtii Mola wao na kufanya matendo yaliyoamrishwa na Mitume.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net