Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 55

Az-Zumar 39:55

الزمر

وَٱتَّبِعُوٓا۟ أَحْسَنَ مَآ أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ ٱلْعَذَابُ بَغْتَةً وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ

Maana

Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyo teremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui. [55]

[55] Na fuateni yaliyo bora kabisa katika mliyo teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi, nayo ni Qur'ani Tukufu, kabla ya kukujieni adhabu kwa ghafla, na bila ya kujitayarisha, na hali nyinyi hamjui kuja kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na fuateni bora zaidi katika kile kilichoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu, nacho ni Qur’ani tukufu, basi jilazimisheni kufuata amri zake na jiepusheni na makatazo yake kabla haijawajia nyinyi adhabu kwa ghafla na nyinyi hamuijui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net