Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 56

Az-Zumar 39:56

الزمر

أَن تَقُولَ نَفْسٌ يَـٰحَسْرَتَىٰ عَلَىٰ مَا فَرَّطتُ فِى جَنۢبِ ٱللَّهِ وَإِن كُنتُ لَمِنَ ٱلسَّـٰخِرِينَ

Maana

Isije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaofanya maskhara!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Isije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyo poteza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanao fanya maskhara! [56]

[56] Rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na Msilimu kwake, na mfuate mafunzo yake, ili nafsi yenye dhambi isisema itapo iona adhabu: Ee msiba wangu kwa niliyo yawacha upande wa Mwenyezi Mungu na katika haki zake, na kwamba mimi nilikuwa duniani miongoni mwa walio kuwa wakiifanyia maskhara Dini yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mtiini Mola wenu na tubieni Kwake ili isije nafsi ikajuta na ikasema, ‘Ee hasara yangu kwa matendo mema niliyoyapoteza ulimwenguni katika yale Aliyoamrisha Allah Mtukufu na nikafanya kasoro katika kumtii na kutekeleza haki yake! Na ingawa ulimwenguni nilikuwa ni miongoni mwa waliokuwa wakiifanyia shere amri ya Allah Mtukufu, Kitabu Chake, Mtume Wake na waliomuamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net