Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 48

Az-Zumar 39:48

الزمر

وَبَدَا لَهُمْ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُوا۟ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Maana

Na utawadhihirikia ubaya wa yale waliyoyachuma, na yatawazingira na kuwafika yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na utawadhihirikia ubaya wa waliyo yachuma, yatawazunguka waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. [48]

[48] Na katika Siku hii ya leo utawadhihirikia uovu wa vitendo vyao, na itawazunguka adhabu ya yale waliyo kuwa wakiyafanyia maskhaara duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yatawadhihirikia hao wakanushaji, Siku ya kuhesabiwa, malipo ya maovu yao waliyoyatenda, kwa kuwa walimnasibishia Allah Mtukufu sifa isiyolingana na Yeye, na wakafanya maasia katika maisha yao, na itawazunguka adhabu kali kila upande, ikiwa ni mateso kwao kwa kulifanyia shere onyo la adhabu ambayo Mtume alikuwa akiwaahidi kuwa itawapata, wakawa hawaitilii maanani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net