Az-Zumar 39:49
الزمرفَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ضُرٌّ دَعَانَا ثُمَّ إِذَا خَوَّلْنَـٰهُ نِعْمَةً مِّنَّا قَالَ إِنَّمَآ أُوتِيتُهُۥ عَلَىٰ عِلْمٍۭ ۚ بَلْ هِىَ فِتْنَةٌ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Na dhara inapomgusa mtu, hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu. Sivyo! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na dhara inapo mgusa mtu hutuomba. Kisha tunapo mpa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya ilimu yangu. Sio! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui! [49]
[49] Na mtu yakimpata madhara hutuomba kwa unyenyekevu; kisha tukimpa neema kwa kumfadhili, mtu huyo huyo husema: Sikupewa neema hizi mimi ila kwa ujuzi wangu nilio nao wa kujua kuchuma. Naye mtu huyu kasahau kuwa mambo si hivyo kama asemavyo, bali neema hizo alizo mneemesha Mwenyezi Mungu ni kama majaribio tu, ni mtihani, ili amdhihirishe nani mwenye kut'ii na nani mwenye kua'si. Lakini wengi wa watu hawatambui kama hayo ni majaribio na fitna.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ikimpata mwanadamu shida na madhara humuomba Mola wake amuondolee, na tunapomuondolea yaliyompata na tukampa neema kutoka kwetu hurudi kumkanusha Mola wake na kukataa wema Wake na huwa akisema, Haya niliyopewa yanatokana na ujuzi wa Allah Mtukufu kuwa mimi ninafaa na ninastahiki kuyapata. Bali huo ni mtihani wa Allah Mtukufu kuwatahini waja Wake, ili Atazame ni yupi anayemshukuru na anayemkanusha. Lakini wengi wao, kwa ujinga wao na dhana zao mbaya, hawajui kuwa hayo ni mavuto kidogo kidogo kutoka kwa Allah Mtukufu na ni mtihani kwao kuhusu kushukuru neema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net