Az-Zumar 39:47
الزمروَلَوْ أَنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مَا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفْتَدَوْا۟ بِهِۦ مِن سُوٓءِ ٱلْعَذَابِ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ وَبَدَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مَا لَمْ يَكُونُوا۟ يَحْتَسِبُونَ
Na lau kuwa wale waliodhulumu wangelikuwa na vyote vilivyomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikomboa kutokana na adhabu mbaya hiyo Siku ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyokuwa wakiyatarajia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa walio dhulumu wangeli kuwa na vyote viliomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikomboa katika adhabu mbaya hiyo Siku ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyo kuwa wakiyatarajia. [47]
[47] Na lau kuwa hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ushirikina wanamiliki vyote viliomo duniani na mara mbili kama hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kuwa ni fidia ya kujigombolea nafsi zao na adhabu waliyo andaliwa Siku ya Kiyama. Nao watakuja iona adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu ambayo haikupata kuwapitikia katika mawazo yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau hao wanaomshirikisha Allah Mtukufu wangekua nacho kila kilichoko kwenye ardhi miongoni mwa mali, vitu vya thamani na vingine mfano wake wangekitoa Siku ya Kiyama ili wajikomboe kwacho na adhabu mbaya. Na lau wangekitoa na wakataka kujikomboa kwacho kisingekubaliwa kutoka kwao na kisingewafaa kitu chochote kuwaepushia na adhabu ya Allah Mtukufu. Na itawadhihirikia wao Siku hiyo amri ya Allah Mtukufu na adhabu zake wasizokuwa wakizidhania duniani kuwa zitawashukia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net