Az-Zumar 39:46
الزمرقُلِ ٱللَّهُمَّ فَاطِرَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ عَـٰلِمَ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِى مَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyo onekana na yanayo onekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika waliyo kuwa wakikhitalifiana. [46]
[46] Ewe Muhammad! Sema, nawe umemwelekea Mola wako: Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Muumba mbingu na ardhi bila ya mithali! Ewe Mjuzi wa siri na dhaahiri! Wewe peke yako, ndiye wa kuhukumu baina ya waja wako katika hayo wanayo khitalifiana katika mambo ya dunia na Akhera. Basi hukumu baina yangu na hawa washirikina!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, «Ewe Allah Mtukufu! Ewe Muumba mbingu na ardhi, Mwenye kuanzisha kuzitengeneza bila kuwa na mfano uliotangulia! Mjuzi wa siri na dhahiri! Wewe unatoa uamuzi baina ya waja wako Siku ya Kiyama katika yale ambayo walikuwa wakitafautiana juu yake ya maneno kuhusu wewe, ukubwa wako, utawala wako na kuhusu kukuamini wewe na kumuamini Mtume wako. Niongoze mimi kwenye haki ambayo watu wametafautiana juu yake, niongoze kwa amri yako. Hakika wewe unamuongoza unayemtaka kwenye njia iliyolingana sawa.» Hii ilikuwa ni miongoni mwa dua za Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), nayo ina mafundisho kwa waja watake himaya kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, na wamuombe kwa mjina Yake mazuri na sifa Zake tukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net