Az-Zumar 39:45
الزمروَإِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَحْدَهُ ٱشْمَأَزَّتْ قُلُوبُ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَإِذَا ذُكِرَ ٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦٓ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ
Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake, nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye, basi wao hufurahi mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anapo tajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasio iamini Akhera huchafuka. Na wanapo tajwa wenginewe asiye kuwa Yeye basi wao hufurahi. [45]
[45] Na pindi akitajwa Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya kutajwa miungu yao, nyoyo za wasio yaamini maisha ya Akhera hukunjana na kukasirika. Na wakitajwa miungu yao wanayo iabudu badala ya Mwenyezi Mungu wao huwa wepesi kufurahi na kustarehe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Anapotajwa Allah Mtukufu Peke Yake zinachukia nyoyo za wasioamini Marejeo na Ufufuzi baada ya kufa, na wanapotajwa wale wasiokuwa Yeye miongoni mwa masanamu, mizimu na wategemewa huwa wakifurahika kwa kuwa ushirikina unaafikiana na matamanio yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net