Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 33

Az-Zumar 39:33

الزمر

وَٱلَّذِى جَآءَ بِٱلصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِۦٓ ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُتَّقُونَ

Maana

Na aliyeuleta ukweli na akausadiki - hao ndio wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na aliye ileta Kweli na akaithibitisha - hao ndio wachamngu. [33]

[33] Na wale walio ileta Haki na wakaisadiki ilipo wajia, hao ndio wachamngu kweli, wala si wengineo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yule aliyekuja na ukweli wa maneno na vitendo, miongoni mwa Manabii na wafuasi wao, na akaukubali kiimani na kivitendo, hao ndio waliokusanya sifa za uchamungu, akiwa mbele yao yule aliye mwisho wa Manabii na Mitume, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wale wenye kumuamini, wanaoifuata Sheria yake kivitendo miongoni mwa Maswahaba, (radhi za Allah Mtukufu ziwashukie), kisha wale wenye kuja baada yao mpaka Siku ya Malipo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net