Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sura ya 39

Az-Zumar

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 33

وَٱلَّذِى جَآءَ بِٱلصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِۦٓ ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُتَّقُونَ 33

{33} Na alipomtaja mwongo anayekadhibisha, uhalifu wake na adhabu yake, akamtaja mkweli anayeaminika na ujira wake, akasema: "Na aliyeuleta ukweli" katika maneno yake na vitendo vyake. Na hapo wakaingia Manabii na waliochukua nafasi zao miongoni mwa wasemao ukweli katika aliyoyasema juu ya habari za Mwenyezi Mungu, hukumu zake na katika yale aliyoyafanya katika sifa za ukweli, "na akausadiki." Kwa sababu mtu anaweza kuja na ukweli, lakini asiusadiki kwa sababu ya kiburi chake au dharau lake kwa yule aliyeusema na akauleta. Kwa hivyo ni lazima ili mtu asifiwe, awe mkweli na mwenye kusadiki. Ukweli wake unaonyesha elimu yake na uadilifu wake, nako kusadiki kwake kunaonyesha unyenyekevu wake na kutotakabari kwake. "Hao" waliowezeshwa kuunganisha mambo mawili haya "ndio wacha Mungu." Kwani sifa zote za uchamungu zinarejea kuwa mkweli katika haki na kuisadiki.