Az-Zumar 39:32
الزمرفَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى ٱللَّهِ وَكَذَّبَ بِٱلصِّدْقِ إِذْ جَآءَهُۥٓ ۚ أَلَيْسَ فِى جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَـٰفِرِينَ
Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uongo Mwenyezi Mungu na akaukadhibisha ukweli ulipomfikia? Je, siyo katika Jahannamu makazi ya hao makafiri?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
BASI NI NANI dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye msingizia uwongo Mwenyezi Mungu na kuikanusha kweli imfikiapo? Je! Siyo katika Jahannamu makaazi ya hao makafiri? [32]
[32] Basi hapana aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye msingizia Mwenyezi Mungu lisio kuwa lake, na akaikanusha Haki bila ya kufikiri wala kuzingatia pale inapo mjia kwa ndimi za Mitume. Kwani katika Jahannamu sio makaazi ya makafiri walio ghurika hata wakamfanyia jeuri Mwenyezi Mungu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna yoyote dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu urongo, kwa kumnasibishia sifa isiyofaa kusifika nayo, kama vile kuwa na mshirika na mtoto, au akasema, «Mimi nimeletewa wahyi,» na hali yeye hakuletewa wahyi wa kitu chochote. Na hakuna dhalimu zaidi kuliko yule aliyeikanusha haki iliyoteremka kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Kwani si yako huko Motoni mashukio na makazi kwa waliomkufuru Allah Mtukufu na wasimuamini Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie)? Ndio, yako.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net