Az-Zumar 39:28
الزمرقُرْءَانًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِى عِوَجٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ
Qur-ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Qur'ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche Mungu. [28]
[28] Tumeiteremsha Qur'ani ya Kiarabu kwa ulimi wao, haina upungufu, kwa kutaraji kuwa watamcha na watamwogopa Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumeijaalia hii Qur’ani ni kwa lugha ya Kiarabu, yenye matamshi yaliyofunuka wazi na yenye maana nyepesi isiyo na uchanganyifu wala upotofu, ili wamche Allah Mtukufu kwa kufuata amri Zake na kuepuka makatazo yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net