Az-Zumar 39:29
الزمرضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا رَّجُلًا فِيهِ شُرَكَآءُ مُتَشَـٰكِسُونَ وَرَجُلًا سَلَمًا لِّرَجُلٍ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana, na wa mtu mwingine aliyehusika na bwana mmoja tu. Je, wako sawa katika hali zao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na bwana mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao? Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui. [29]
[29] Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mshirikina kama mtumwa aliye milikiwa na watu kadhaa wenye kushirikiana, na wenye kumgombania. Na mfano wa mwenye kuamini Mwenyezi Mungu Mmoja kama mtu ambaye amemilikiwa na mtu mmoja tu. Je hao wanakuwa sawa? Alhamdulillahi kwa kusimama hoja mbele ya watu. Lakini watu wengi hawaijui Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Anapiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa na washirika wenye kuvutana, na mtumwa mwingine aliyekuwa ni wa mmiliki mmoja tu, akawa yuwajua matakwa yake na yanayomridhisha. Je, mfano wa wawili hao unalingana? Basi hivyo ndivyo alivyo mshirikina. Yeye yuko katika hali ya mshangao na shaka, na Muumini yuko katika raha na utulivu. Sifa njema kamilifu zilizotimia ni za Allah Mtukufu, Peke Yake, lakini washirikina hawaijui haki wakaifuata.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net