Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sura ya 39

Az-Zumar

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 28

قُرْءَانًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِى عِوَجٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ 28

{28} "Qur-ani ya Kiarabu isiyo na upogo." Yenye lafudhi zilizo wazi, yenye maana nyepesi, haswa kwa Waarabu, na isiyokuwa na kasoro wala upungufu kwa namna yoyote ile, katika lafudhi zake wala katika maana zake. Hili linalazimu kwamba imenyooka kikamilifu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo. Kimenyooka sawa." "Ili wamche Mungu" Mtukufu, kwa kuwa tumewarahisishia njia za kielimu za ucha Mungu na za kivitendo za ucha Mungu kwa Qur-ani hii ya Kiarabu iliyonyooka, ambamo Mwenyezi Mungu amepiga kila mifano.