Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 69

Yaseen 36:69

يس

وَمَا عَلَّمْنَـٰهُ ٱلشِّعْرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُۥٓ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْءَانٌ مُّبِينٌ

Maana

Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu isipokuwa ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha. [69]

[69] Na Sisi hatukumfunza Mtume kutunga mashairi. Wala haifai hivyo, kwa kuzingatia pahala pake na cheo chake awe mtungaji mashairi! Hii Qur'ani iliyo teremka juu yake si chochote ila ni mawaidha, na Kitabu cha mbinguni kilio wazi. Hakikhusiani kabisa na mashairi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hatukumfundisha mjumbe wetu Muhammad mashairi, na haipasi kwake kuwa mshairi. Haikuwa hii aliokuja nayo isipokuwa ni Ukumbusho kwa wale wenye busara kujikumbusha nao na ni Qur’ani yenye kufafanua haki na batili, hukumu zake ziko wazi, na pia hekima zake na mawaidha yake yako wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net