Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 70

Yaseen 36:70

يس

لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri. [70]

[70] Hii Qur'ani ni kumtia khofu mwenye moyo ulio hai ulio nawirika kwa akili. Na ipite hukumu ya adhabu kuwashukia wanao ipinga Qur'ani, wenye kukataa uwongofu wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ili imuonye ambaye moyo wake uko hai na akili yake ina nuru, na ili ithibiti adhabu kwa wenye kumkanusha Allah Mtukufu, kwa kuwa wao, kwa hii Qur’ani, hoja ya Allah Mtukufu ya mkato imewasimamia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net