Faatir 35:32
فاطرثُمَّ أَوْرَثْنَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلَّذِينَ ٱصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌۢ بِٱلْخَيْرَٰتِ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَضْلُ ٱلْكَبِيرُ
Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateua miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliyejidhulumu, na yupo wa katikati, na yupo aliyetangulia katika mambo ya heri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateuwa miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliye tangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu. [32]
[32] Tena tumekifanya Kitabu hichi ni mirathi ya kurithiwa na waja wetu tulio wateuwa. Basi kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake kwa kuzidi maovu yake kuliko mema yake; na yupo wa kiasi, hakupita mpaka katika maovu yake na wala hakukithirisha mema yake; na miongoni mwao yupo aliye washinda wenginewe kwa kufanya mambo ya kheri, kwa kusahilishiwa na Mwenyezi Mungu. Huko kushinda katika mambo ya kheri ndio kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha tukawapa Qur’ani, baada ya ummah waliopita kuangamia, wale tuliowachagua miongoni mwa umati wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie): kati yao kuna aliyeidhulumu nafsi yake kwa kufanya baadhi ya maasia, na kati yao kuna aliyekuwa wastani, naye ni yule mwenye kutekeleza yaliyo wajibu na kuepuka yaliyoharamishwa, na katika wao kuna mwenye kutangulia kufanya mambo ya kheri kwa idhini ya Allah Mtukufu, yaani mwenye kukimbilia na kujitahidi kufanya amali njema, za faradhi na za ziada. Na kupewa Kitabu huko na kuchaguliwa ummah huu ndio fadhla kubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net