Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 33

Faatir 35:33

فاطر

جَنَّـٰتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ

Maana

Mabustani ya milele watayaingia. Huko watavikwa vikuku vya dhahabu na lulu, na nguo zao humo ni za hariri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mabustani ya milele watayaingia. Huko watavikwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na nguo zao humo ni za hariri. [33]

[33] Malipo yao Akhera ni Mabustani ya daima watayo yaingia. Humo watajipamba kwa vikuku vya dhahabu na lulu. Na nguo zao za Peponi ni hariri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wataingia pepo ya makazi ya daima kwa wale ambao Allah Mtukufu Amewarithisha Kitabu Chake, watapambwa huko kwa vidani vya dhahabu na kwa lulu. Na mavazi yao ya kawaida huko Peponi ni hariri, yaani: nguo laini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net