Faatir 35:31
فاطروَٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ هُوَ ٱلْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِعِبَادِهِۦ لَخَبِيرٌۢ بَصِيرٌ
Na hayo tuliyokufunulia kutoka Kitabuni ni Kweli, yenye kusadikisha yale yaliyokuwa kabla yake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye habari na Mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hayo tuliyo kufunulia kutoka Kitabuni ni Kweli yenye kusadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye khabari na Mwenye kuona. [31]
[31] Na tuliyo kuletea Wahyi wewe katika hii Qur'ani ni Haki tupu isiyo kuwa na shaka yoyote. Tumeiteremsha kuthibitisha Vitabu vilivyo teremshwa kwa Mitume walio kuwa kabla yako, kwa kuwa vyote ni asli moja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa kujua na kuona kwa waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Qur’ani tuliyokuteremshia wewe, ewe Mtume, ndiyo haki inayosadikisha Vitabu Alivyoviteremsha Allah Mtukufu kwa Mitume Wake kabla yako. Hakika Allah Mtukufu ni Mtambuzi wa mambo ya waja Wake, ni Mwenye kuviona vitendo vyao, na Atawalipa wema kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net