Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 30

Faatir 35:30

فاطر

لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ غَفُورٌ شَكُورٌ

Maana

Ili Yeye awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ili Yeye awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani. [30]

[30] Ili Mwenyezi Mungu awalipe ujira wao, na awazidishie juu yake kutokana na fadhila yake kwa anavyo waongezea mema yao na kuwafutia maovu yao. Yeye ni Msamehevu, Mwingi wa kufutia makosa ya kujikwaa, Mwenye kushukuru, Mwingi wa kushukuru kwa ut'iifu wa waja.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ili Awatimizie Allah Mtukufu, Aliyetukuka, malipo mema ya matendo yao yakiwa kamili bila kupunguzwa, na wataongezewa mema kwa fadhila Zake. Hakika Allah Mtukufu ni msamehevu sana wa makosa yao, ni Mwingi wa shukrani kwa mema yao, Atawalipa kwa mema hayo malipo mazuri mengi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net