Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 29

Faatir 35:29

فاطر

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَـٰبَ ٱللَّهِ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُوا۟ مِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَـٰرَةً لَّن تَبُورَ

Maana

Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Swala, na wakatoa kwa siri na kwa dhahiri katika vile tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyobwaga.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Swala, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika tulivyo waruzuku, hao hutaraji biashara isiyo bwaga. [29]

[29] Hakika wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa kukizingatia na kukitenda, na wakashika Swala kwa mujibu itakikanavyo na wakatoa kwa siri na kwa kuonekana baadhi ya alicho waruzuku Mwenyezi Mungu, wanataraji kwa hayo kufanya na Mwenyezi Mungu biashara isiyo anguka faida yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika ya wale wanaosoma Qur’ani na wakaifanyia kazi, wakaendelea daima kuswali kwa nyakati zake na wakatumia kile tulichowaruzuku miongoni mwa aina ya matumizi ya lazima na ya yanayopendekezwa, kwa siri na kwa dhahiri, hao wana matumaini kwa hayo kufanya biashara isiyoisha na isiyoanguka, nayo ni kuridhiwa na Mola wao na kufaulu kupata malipo mengi mema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net