Faatir 35:28
فاطروَمِنَ ٱلنَّاسِ وَٱلدَّوَآبِّ وَٱلْأَنْعَـٰمِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهُۥ كَذَٰلِكَ ۗ إِنَّمَا يَخْشَى ٱللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ ٱلْعُلَمَـٰٓؤُا۟ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ
Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinahitalifiana. Kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe. [28]
[28] Na miongoni mwa watu na wanyama, na mifugo, yaani ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi, kadhaalika zipo khitilafu katika sura, ukubwa na rangi. Na hawazingatii huu muumbo wa ajabu na wakamwogopa aliye umba ila wanazuoni ambao wanatambua siri ya uumbaji wake. Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda anaogopwa na Waumini, naye ni Mwingi wa kuwafutia madhambi yao wanao rejea kwake. Baada ya kueleza kukhitalifiana matunda, na milima, na watu, na wanyama, na mifugo, inaashiriwa kuwa juu ya khitilafu hizi zinazo onekana baina ya hali hizi zote, upo umoja wa asli. Kwani hayo matunda yanatokana na maji yale yale. Na milima inatokana na Magma moja. Kadhaalika khitilafu za rangi, na watu, na wanyama, na mifugo, hazidhihiri katika tone za manii ambavyo vyote hivyo vimetoka mwanzo wake. Na lau hizo tone zingeli chunguzwa kwa darubini ya Maikroskopu kisingeli onekana kitu cha kuonyesha hizo khitilafu zitazo kuwa. Kwani hizo ni siri zilioko ndani yake katika zinazo itwa Genes (Jiinz). Na labda haya pia yanaonyesha kuwa sifa za kurithi ziliomo katika asli ya mimea, na wanyama, na binaadamu, zinalindwa katika maumbile yake, na hazigeuki kwa tabia ya pahala au chakula.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa watu na wanyama, ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo tumeumba wakiwa rangi tofauti vilevile. Kati ya hao kuna wekundu, weupe, weusi, na wenye rangi nyinginezo, kama vile kutofautiana rangi za matunda na majabali. Hakika wanaomcha Allah Mtukufu na kujikinga na mateso Yake kwa kumtii na kujiepusha kumuasi ni wale wanaomjua Yeye, (kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake), sifa Zake na Sheria Zake, na uwezo Wake juu ya kila kitu ambao miongoni mwavyo ni kutofautiana viumbe hivi pamoja na kuwa sababu yake ni moja, na wanayatia akilini yaliyomo ndani ya mawaidha na mazingatio. Hakika Allah Mtukufu ni Mshindi Mwenye nguvu Asiyeshindwa, Mwingi wa kusamehe, Anawapa malipo mema watiifu, na Anawasamehe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net