Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 27

Faatir 35:27

فاطر

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَخْرَجْنَا بِهِۦ ثَمَرَٰتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَٰنُهَا ۚ وَمِنَ ٱلْجِبَالِ جُدَدٌۢ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ

Maana

Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu aliteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tukayatoa matunda yenye rangi mbalimbali. Na katika milima zimo njia nyeupe na nyekundu, na rangi mbali mbali, na milima mieusi sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana. [27]

[27] Ewe mwenye akili! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu anayateremsha maji kutoka mbinguni, na kwa maji hayo anatoa mazao yanayo khitalifiana rangi zake? Mengine ni mekundu na manjano, na matamu na machungu, mazuri na mabaya. Na katika milima, ipo milima yenye njia na mistari myeupe na myekundu, yenye kukhitalifiana pia kwa kukoza na kufifia. Ya kustaajabisha kitaalamu katika Aya hii tukufu sio tu kwa kukhitalifiana rangi mbali mbali katika milima, ambazo zinatokana na hizo sehemu za maadini zilizo fanya majabali, kama vile chuma huonyesha rangi yake nyekundu, na manganese na makaa ya mawe huonekana kwa rangi nyeusi, au shaba ambayo hudhihirisha rangi ya kijani n.k. Lakini ya kustaajabisha khasa ni kuunganisha baina ya kutoa matunda ya namna mbali mbali na hali miti yake inanyweshwa maji yale yale, na kuumbwa milima myekundu, na myeupe, na myeusi, na yote yana asli moja kwa kuundwa kwake. Wataalamu wa ilimu za t'abaka za ardhi, Jiolojia, wanaita Magma. Na hii Magma moja inapo chomoza pahala mbali mbali katika ardhi, na penye vina mbali mbali (kwenda chini) katika ardhi kutoka juu basi hupatikana khitilafu katika muundo wake na hukusanyika kwa kurindika kuwa ni milima yenye maadini ya rangi mbali mbali. Na huu basi mwendo wa Mwenyezi Mungu ni mmoja. Kwani hakika asli ni moja, na matawi ndiyo yanakhitalifiana kwa kuonekana. Na katika haya yanapatikana manufaa na faida kwa binaadamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani huoni kwamba Allah Mtukufu Ameteremsha kutoka juu maji, tukainywesha kwayo miti iliyo ardhini, tukatoa kwenye miti hiyo matunda yenye rangi tofauti, miongoni mwazo ni nyekundu na miongoni mwazo nyeusi na manjano na zisizokuwa hizo? Na tumeumba majabalini njia zenye rangi tofauti, nyeupe na nyekundu. Na tumeumba miongoni mwa majabali, majabali meusi sana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net