Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 48

Saba 34:48

سبإ

قُلْ إِنَّ رَبِّى يَقْذِفُ بِٱلْحَقِّ عَلَّـٰمُ ٱلْغُيُوبِ

Maana

Sema: "Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema ya ghaibu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa Haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema yaliyo ghaibu. [48]

[48] Waambie: Hakika Mola wangu Mlezi huitupa Haki juu ya baat'ili (uwongo) ikauondoa. Na Yeye ndiye Mwenye kuijua vyema ghaibu; hapana siri inayo fichikana kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, umwambie anayekanusha upwekeshaji wa Allah Mtukufu na ujumbe wa Uislamu, «Hakika Mola wangu Anauvurumiza ubatilifu kwa hoja za ukweli, hivyo basi ukaufedhehi na ukauangamiza. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi mno wa vitu visivyoonekana, hakuna kinachofichika Kwake chochote ardhini na mbinguni».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net