Saba 34:47
سبإقُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ
Sema: "Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ujira nilio kuombeni ni wenu nyinyi. Sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu. [47]
[47] Waambie makafiri: Ujira wowote nilio kutakeni juu ya kufikisha Ujumbe ni kwa maslaha yenu. (Yaani nyinyi mwongoke na mpate malipo kwa Mwenyezi Mungu.) Sina ujira ninao utaraji mimi ila kwa Mwenyezi Mungu. Naye ni Mwenye kuangalia na kuchungua kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, uwaambie wakanushaji, «Malipo niliyowaomba kwa wema huu niliowaletea ni yenu nyinyi. Malipo yangu mimi ninayoyangojea hayapo isipokuwa kwa Allah Mtukufu Mwenye kuyaona matendo yangu na matendo yenu. Hakuna chochote kinachofichika Kwake. Yeye Anawalipa wote: kila mmoja kwa anachostahiki».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net