Saba 34:46
سبإقُلْ إِنَّمَآ أَعِظُكُم بِوَٰحِدَةٍ ۖ أَن تَقُومُوا۟ لِلَّهِ مَثْنَىٰ وَفُرَٰدَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا۟ ۚ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ لَّكُم بَيْنَ يَدَىْ عَذَابٍ شَدِيدٍ
Sema: "Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote isipokuwa ni mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali. [46]
[46] Waambie: Mimi nakuamrisheni jambo moja tu - Msimame kwa ikhlasi ya kumtakasia Mwenyezi Mungu muache kufuata mitindo yenu ya zamani - katika kuchungua kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, mkigawika wawili-wawili, au mmoja-mmoja, muangalie kwa uadilifu na insafu. Kisha mfikiri khabari ya huyu mwenzenu, Muhammad, ambaye mmeishi naye na mnajua kuwa akili yake ni timamu. Huyu hana wazimu kwa kuliingia jambo hili. Yeye huyu si chochote ila ni Mwonyaji kwenu, anakuhadharisheni msije mkapata adhabu kali inayo kukabilini mbele yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa wakanushaji washindani, «Mimi ninawapa ushauri mmoja: msimame kumtii Allah Mtukufu wawili wawili na mmoja mmoja, kisha mfikirie kuhusu hali ya mwenzenu, Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kile alichonasibishwa nacho. Yeye hana wazimu. Hakuwa Yeye isipokuwa ni mwenye kuwaonya na adhabu ya Jahanamu kabla joto lake halijawasumbua».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net