Saba 34:45
سبإوَكَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَمَا بَلَغُوا۟ مِعْشَارَ مَآ ءَاتَيْنَـٰهُمْ فَكَذَّبُوا۟ رُسُلِى ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ
Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walikadhibisha walio kuwa kabla yao. Na hawakufikilia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyo wapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani! [45]
[45] Na kaumu zilizo tangulia ziliwakadhibisha Manabii wao. Na hawa washirikina wa kaumu yako hawajafikia hata sehemu moja katika kumi za nguvu na umadhubuti tulio wapa hao walio tangulia. Wakawakanusha Mitume wangu. Basi ilikuwaje ghadhabu yangu juu yao jinsi nilivyo wakasirikia!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walikanusha wale waliokuwa kabla yao, kama vile ‛Ᾱd na Thamūd, Na watu wa Makkah hawakufikia ushuri wa kile tulichowapa ummah waliopita cha nguvu, wingi wa mali, umri mrefu na neema nyiginezo, na tukawaangamiza. Basi angalia, ewe Mtume! Ni namna gani yalivyokuwa makemeo yangu na adhabu yangu kwao?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net