Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 49

Saba 34:49

سبإ

قُلْ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ ٱلْبَـٰطِلُ وَمَا يُعِيدُ

Maana

Sema: "Kweli imefika, na batili haijitokezi, wala hairudi."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Kweli imefika, na uwongo haujitokezi, wala haurudi. [49]

[49] Waambie: Uislamu umedhihiri, wala uwongo hauwezi kuwa ndio njia ya kuipinga Haki. Na hizo mbinu za zamani hazirejei tena.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, «Ukweli na Sheria tukufu itokayo kwa Allah Mtukufu umekuja, na ubatilifu umeondoka na mamlaka yake yamepotea, hivyo basi ubatilifu haukusaliwa na kitu cha kukianzisha wala kukirudisha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net