Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 42

Saba 34:42

سبإ

فَٱلْيَوْمَ لَا يَمْلِكُ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ نَّفْعًا وَلَا ضَرًّا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلنَّارِ ٱلَّتِى كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ

Maana

Basi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe. Na tutawaambia wale waliodhulumu, "Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenzie. Na tutawaambia walio dhulumu: Onjeni adhabu ya Moto mlio kuwa mkiukanusha. [42]

[42] Basi Siku ya Mkusanyo hapana atakaye weza kumletea mwenzie manufaa wala kumkinga na madhara. Na tutawaambia walio jidhulumu nafsi zao: Ionjeni adhabu ya Moto ambayo mlio kuwa duniani mkiikanusha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Siku ya Ufufuzi, hao waabudiwa hawatakuwa na mamlaka ya kuwanufaisha au kuwadhuru wenye kuwaabudu. Na tutasema kuwaambia wale waliozidhulumu nafsi zao, «Onjeni adhabu ya Moto ambao mlikuwa mkiukanusha!»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net