Saba 34:41
سبإقَالُوا۟ سُبْحَـٰنَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِم ۖ بَلْ كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ ٱلْجِنَّ ۖ أَكْثَرُهُم بِهِم مُّؤْمِنُونَ
Waseme, "Subhanak (umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waseme: Subhanak, Umetakasika. Wewe ndiye kipenzi chetu si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao. [41]
[41] Malaika watasema: Sisi tunakutakasa kabisa na kuwa Wewe una mshirika wowote. Wewe ndiye tulio shikamana nawe kwa mapenzi na ut'iifu, sio wao. Hao wameghurika katika madai yao kuwa wanatuabudu sisi. Bali walikuwa wanafuata nyayo za mashetani walio wapambia ushirikina. Wengi wao wakiwasadiki hao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Malaika watasema, «Tunakutakasa, ewe Allah Mtukufu, na kuwa na mshirika wa kuabudiwa! wewe Ndiye Msimamizi wetu tunayemtii na kumuabudu Peke Yake. Bali hawa walikuwa wakiwaabudu mashetani, wengi wao wanawaamini na kuwatii».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net