Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 43

Saba 34:43

سبإ

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُنَا بَيِّنَـٰتٍ قَالُوا۟ مَا هَـٰذَآ إِلَّا رَجُلٌ يُرِيدُ أَن يَصُدَّكُمْ عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ ءَابَآؤُكُمْ وَقَالُوا۟ مَا هَـٰذَآ إِلَّآ إِفْكٌ مُّفْتَرًى ۚ وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ

Maana

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wanasema: "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu." Na wakasema: "Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa." Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi wanasema: Huyu si chochote ila ni mtu anaye taka kukuzuieni na waliyo kuwa wakiabudu baba zenu. Na wakasema: Haya si chochote ila ni uwongo ulio zuliwa. Na walio kufuru waliiambia Haki ilipo wajia: Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhaahiri. [43]

[43] Na makafiri walipo somewa Aya zetu zilio wazi dalili zake kuonyesha Haki, makafiri walisema: Huyu si chochote ila ni mtu anaye taka kukuzuilieni msiwaabudu walio kuwa wakiwaabudu baba zenu. Na pia walisema: Hii Qur'ani si chochote ila ni uwongo ulio tungwa tu. Na walio ikataa Qur'ani ilipo wajia walisema: Hii si chochote ila ni uchawi ulio wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wanaposomewa makafiri wa Makkah aya za Allah Mtukufu zikiwa wazi wanasema, «Hakuwa Muhammad isipokuwa ni mtu anayependa kuwakataza nyinyi kuwaabudu waungu ambao baba zenu walikuwa wakiwaabudu,» na wanasema, «Haikuwa hii Qur’ani isipokuwa ni urongo uliozuliwa, umeuleta wewe mwenyewe na sio kuwa unatoka kwa Allah Mtukufu.» Na makafiri walisema kuhusu Qur’ani ilipowajia, «Haikuwa hii isipokuwa uchawi uliojitokeza wazi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net