Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 39

Saba 34:39

سبإ

قُلْ إِنَّ رَبِّى يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ وَيَقْدِرُ لَهُۥ ۚ وَمَآ أَنفَقْتُم مِّن شَىْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُۥ ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Maana

Sema: "Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakachokitoa, Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakacho kitoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanao ruzuku. [39]

[39] Ewe Nabii! Sema: Hakika Mola wangu Mlezi anamkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha amtakaye. Na chochote mtacho kitoa Yeye atakilipa. Na Yeye Aliye takasika ni Mbora wa wenye kuruzuku.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, hawa waliodanganyika kwa mali na watoto, Mola wangu anamkunjulia riziki Anayemtaka miongoni mwa waja Wake na anampunguzia Anayemtaka, kwa hekima Anayoijua. Na namna mtakavyotoa kitu chochote, Yeye Atawapa badala yake duniani na huko Akhera Atawapa malipo mema. Na Yeye, (kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake), Ndiye bora wa wenye kuruzuku, basi tafuteni riziki Kwake Peke Yake, na zungukeni kwa kufuata sababu zake Alizowaamuru.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net