Saba 34:38
سبإوَٱلَّذِينَ يَسْعَوْنَ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا مُعَـٰجِزِينَ أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى ٱلْعَذَابِ مُحْضَرُونَ
Na wale wanaojitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanao jitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu. [38]
[38] Na hao ambao wana fanya juhudi kuzipinga Ishara zetu, wakifanya kila hila kuzivunja na kuwazuia Manabii wetu wasifikishe Ujumbe wake, hao, basi watakuwa katika adhabu, wamehudhurishwa na wala hawataepuka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wanaokimbilia kuzibatilisha hoja zetu na wanaozuia njia ya Allah Mtukufu isifuatwe wakiwa wapinzani na washindani, hawa wataingia ndani ya adhabu ya Jahanamu Siku ya Kiyama, watajiwa na Zabāniyah, ambao ni askari wa Motoni, na hawatatoka humo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net